Kalunde Jamal IKIWA
ni mwezi wa sita ambapo kwa kawaida mwezi huu unaugawa mwaka , kwa
binaadamu mwenye malengo huwa tayari anajua nini muelekeo wake na nini
amevuna.
Kutokana hilo msanii, Nassib Abdul a.k.a Diamond
ambaye tangu kuanza kwa mwaka huu amekuwa akiwika ndani na nje ya nchi,
anazungumza kiundani katika kipindi hiki amefanikiwa kiasi gani.
Starehe:Hongera sana kwa kuugawa mwaka salama.
Diamond:Nashukuru sana kwani siku hizi kifo kipo mkononi.
Starehe:Tukiwa tunaugawa mwaka na wewe ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri mwaka huu labda siri ya mafanikio yako ni nini?
Diamond:Kiukweli
siri ya mafanikio yangu ni kujituma kwa bidii lakini zaidi ni malengo
ambayo hujiwekea kabla ya mwaka kuisha kwamba mwakani nitafanya hivi na
hivi.
Starehe: Kwa maana hiyo unataka kusema mafanikio yako uliyatarajia?
Diamond:Kulingana
na mipango yangu na malengo niliyojiwekea mwaka jana ni kama nilikuwa
nawaza kupata mafanikio ingawa kwa kiasi kikubwa nilitegema zaidi
mashabiki watakavyonipokea bila kusahau nini nitawapa.
Starehe:Enhee....
Diamond:Hiyo
ndio siri pekee pamoja na kutegemea mashabiki lakini pia nilisoma soko
la muziki linataka nini si unajua sasa hivi Dunia ni kama
kijiji,kinachoimbwa Marekani kinakuja huku kwetu kama upepo lakini kuna
nchi jirani ambazo kwa kiasi fulani tabia zetu zinafanana, hivyo hata
ujumbe uliopo kwenye tungo zetu unaendana japo sio sana.Kabla ya kutoa
wimbo ili mashabiki waupende inabidi uangalie mambo kama hayo.
Starehe:Unaonaje ushindani wa muziki kwa majirani zetu, yaani Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda n.k
Diamond:Kwanza
kabisa nakuhakikishia kwa nchi za Afrika Mashariki Tanzania tupo vizuri
kimuziki na ndio maana tunakubalika nchi zote tano,nasema hivyo kwa
kuwa wanamuziki ambao tunafanya vizuri hapa nyumbani tupo wengi tofauti
na nchi nyingine kati ya hizo tano ambazo labda msanii anayetamba ni
mmoja mmoja.
Starehe:Mbona umejibu kwa kujiamini unaweza kunipa mfano hata mmoja kuthibitisha hilo?
Diamond:....Kicheko...mifano
ipo mingi lakini mmojawapo ni kwamba hawezi kuja msanii kutoka kati ya
nchi hizo akapata mashabiki wengi kutoka kwetu bila kushirikiana na
wanamuziki wa hapa nyumbani, hiyo inaonyesha kuwa hawana uwezo kushinda
sisi na ndio maana waandaji wamelitambua hilo na kuhakikisha akija
mwanamuziki na wenyewe tunakuwepo ili kuwapa raha mashabiki wetu. Sisi
tuna uwezo wa kwenda nchi nyingine na kupiga shoo bila kumshirikisha
msanii kutoka nchi tuliyoenda.
Starehe:Hongera sana kwa niaba ya
wanamuziki wenzako,lakini turudi kwako wewe binafsi ni shoo gani kali
umepiga tangu kuanza kwa mwaka huu hadi kufikia sasa?
Diamond:Tabasamu
pana....Kiukweli zipo mbili na nikitaja moja nitawapunja mashabiki
wangu ambao kwa nia moja ama nyingine wananiunga mkono kila ninapofanya
shoo.
Starehe:Mmh...ni zipi hizo Diamond?
Diamond:Nashukuru
kwa kupata nafasi hii kwanza kabisa nawashukuru mashabiki wangu kwa
jinsi walivyoniunga mkono katika shoo hizo,ambazo ni ile niliyopiga
Mlimani
City ambayo niliipa jina la Diamond Are Forever,na ile
niliyopiga Mbagala katika Ukumbi wa Dar Live kiukweli sitazisahau na
ninasema ahsante sana mashabiki wangu.
Starehe:Bado hujatueleza vizuri kwa nini huwezi kuzisahau na unajivunia kuwa mwanamuziki kwa shoo hizo tangu mwaka huu uanze ?
Diamond:Huwezi
amini kwenye shoo ya Mlimani City nilikusanya zaidi ya sh80mil za
Tanzania na ya Mbagala nililipwa sh10mil bila utata wala longolongo
yoyote.
Starehe:Zaidi ya kukusanya fedha nyingi nini kilikufurahisha na kujivunia.
Diamond:Sikufichi
ni shoo ya Mbagala,kwa sababu ni shoo iliyokutanisha watu wa rika zote
wakubwa, watoto,vijana na watu wa makamu walionifurahisha zaidi ni
watoto kwa kuwa waliweza kunisubiri na hii ni faraja kwangu kwa kuwa
nimeona ni kwa jinsi gani ninapendwa na kutoa burudani kwa watu wa rika
zote nimefurahishwa sana na hilo.
Starehe:Kutokana na kiwango
chako kupanda na hivi majuzi umepaform kwenye jumba la Big Brother ni
wasanii Wangapi wa nje ambao wametaka kufanya kolabo na wewe.
Diamond:Hata
kabla ya kwenda Big Brother ambayo na hiyo ni moja ya mafanikio
kwangu,wasanii wengi wa nje ingawa sipendi kuwataja walikuwa wananiomba
nifanye nao kolabo lakini kuna mambo yalinifanya niwe bize kidogo
nikikaa vizuri kila kitu kitakuwa poa.
Starehe:Pamoja na mafanikio uliyoyapata wewe binafsi lakini hali ya muziki unaionaje.
Diamond:Nikitoa
kulinganisha na nchi nyingine kama nilivyokujibu mwanzo, muziki unakuwa
huku changamoto ikiwa kubwa kwa wanamuziki wakongwe kwa kuwa kuna
wanamuziki wanaibuka, ingawa hawadumu kwenye fani lakini akitoa nyimbo
inakuwa juu sasa kama hujasimama imara lazima uyumbe.
Starehe:Ndio unataka kusemaje hasa kwa hao wanaoingia na kutoka na kwa nyinyi wakongwe.
Diamond:Wanaoingia
na kutoka sina komenti kwa kuwa labda hawakujipanga, kazi inabaki kwa
wakongwe kuhakikisha wanapambana na changamoto hii,kwani kutolewa nishai
na mwanamuziki chipukizi ni aibu.
Starehe:Mashabiki wako wategemee nini mwezi huu ambapo tupo katikati ya mwaka 2012.
Diamond:Kwanza
kabisa kabla ya yote wakae mkao wa kula kupokea video ya wimbo wa 'Lala
salama' na nimpende nani,nasema ni kali narudia tena ni kali wakae mkao
wa kuburudika roho ,mwili,akili na macho pia kwa kuona kitu kizuri. HABARI NA SPORT STAREHE | | |
No comments:
Post a Comment