Ilikuwa
kama muvi vile ndugu hawa walipoanza kusimulia kupitia clouds media
jinsi ya wao walivyojiunga na mlengwa wa kushoto wa maisha kama watu
wanavyodai hapa tukizungumzia Kuabudu freemason kwenye maisha yao.
Kwenye maelezo yao hawa jamaa inaonekana kabisa hawakujipanga kutoa
taarifa zilizo rasmi kwani walikuwa wakikinzana kwenye kutoa maelezo
waliyodhamiria kuyatoa ambapo walikuwa wakieleza jinsi mlengwa huo
unavyofanya kazi na wao wakiwa kama wafuasi wa mlengwa huo ambapo
walitinga studioni mwa Clouds media wakiwa na laptop yao iliyoonesha
baadhi ya mambo.
Lakini wakati wa mahojiano
na Zamaradi Mketema walieleza kuwa mwanachama wa mlengwa huoni wa dini yeyote aidha awe Muislamu au Mkristo na ndipo lilipokuja swali kwamba "Basi mwanachama wa mlengwa huo na kundi lake hawana ibada?" wakajibu huwezi kuwa Mromani kama hufanyi ibada za Kiromani!
Hivyo freemason lazima aje kwa ibada na kushindwa kueleza hasa mlengwa huo unavyofanya kazi zake,!! Picha ni za jamaa hao wakiwa wanahojiwa wakati wa kipindi cha leo tena cha Dinna.
No comments:
Post a Comment