Waziri
wa Usalama wa ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode
wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo
asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa
ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Abiria
wote saba waliokuwa kwenye ndege hiyo wanaarifiwa kuteketezwa kwa kiasi
cha kutoweza kutambulika. Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu
katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la
Sotik kwa mkutano wa usalama.
Saitoti
alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa
wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka
angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong.
Polisi
wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere
aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana
na ajali hiyo...
source/bbc
No comments:
Post a Comment